Salama Na podcast

SE7EP37 - SALAMA NA TOUFIQ | Um'PENDAE

23.2.2023
0:00
35:56
15 Sekunden vorwärts
15 Sekunden vorwärts

Toufiq ni moja ya majina makubwa kati ya wafanya biashara wazuri na sasa mwanasiasa na Mbunge wa Mpendae, kwa wazee na vijana wa visiwani humo yeye ni mmoja wa mifano ya kuigwa ingawa kwake yeye yaliyo mengi kwenye maisha yake ni nguvu kubwa ilifanywa na Marehemu Mzee wake Ndugu Salih Hassan Abdullah Turky aka Mr White ambaye na yeye akiacha ukweli kwamba alikua tajiri na mfanya biashara nzuri huko visiwani ila yeye pia alikua kipenzi cha wananchi wa Jimbo la Mpendae ambapo sasa Toufiq ndo anaye liongoza jimbo hilo baada ya Mzee wake kutangulia mbele ya haki. Mwenyezi Mungu Amrehemu.


Kwenye meza yetu ya kigae na kiti chetu kikukuu Taufiq anakumbuka wakati wa msiba wa Mzee wake bado wa moto kabisa watu walikua wanakuja nyumbani kwao na kumshauri yeye agombee ubunge wa jimbo hilo ambalo Mzee wake alikua akiliongoza. Ikumbukwe Mzee wake Mr White alifariki kipindi ambacho wananchi walikua wanajiandaa kwa uchaguzi wa wabunge wawakilishi na Rais, ananiambia kwanza aliwafukuza watu hao, wakarudi tena baada ya maziko bado Toufiq akawakatalia, baadae baada ya mambo kutulizana na kuombeleza kupungua watu ambao anawaheshimu walimfuata tena na kumueleza umuhimu wa yeye kugombea jimbo hilo. Wakamuelezea umuhimu wa Marehemu Mzee wake kwa watu wa Mpendae na kwamba kama hatofanya hivyo basi haitakua jambo zuri kwa wakazi wa eneo hilo. Ndugu Turky ilibidi akubaliane na ombi hilo na kutimiza matakwa ya wana Mpendae ambao walimpa kura nyingi za ndio.


Yeye mawazo yake yalikua kwenye kuendeleza biashara zaidi ambayo kwa kiasi kikubwa Mzee wake alikua alimshirikisha nayo toka akiwa mdogo. Kuweza kufanya yote hayo kwa kijana mdogo kama yeye pengine ingekua mambo mengi sana so kwa heshima wakati mambo mengine yanaenda Toufiq ilibidi aachie majukumu mengine kwa Mdogo wake wa Kiume Ndugu Abdallah Salim na Dada yake Bi Khaytham Salim Turky, ingawa bado yeye ndo Mwenyekiti wa makampuni hayo ambayo yamejikita katika biashara mbali mbali ambazo zimestawi visiwani Zanzibar na nchi nyengine.


Toufiq alikuja kwenye maongezi haya akiwa na mambo yake mengine ya ki majukumu kwenye meza yake na ki ukweli hatukupata wasaa teeele wa kuweza kuyachambua mengi kama ambavyo tungependa lakini pia hatukukosa lolote jambo la lolote jambo hilo ndo tumaini letu litasaidia kwenye kukusogeza kwenye sehemu fulani katika uelewa na uchambuzi wako wa mambo.

Tafadhali enjoy hiki kidogo ambacho tuliweza kukukusanyia kwenye muda mchache.


Love,

Salama.

--- Support this podcast: https://podcasters.spotify.com/pod/show/yahstonetown/support

Weitere Episoden von „Salama Na“