Ushawahi kumuangalia mtu kwa mbali na kujiuliza maswali mengi juu yake? Maswali kama siku yake ikoje, amewezaje? Kama ana familia? Ki kawaida huwa anaamka saa ngapi? Amesoma wapi? Siku yake anaipangaje? Ana watoto? Mtoto? Huwa anawaandaa kwenda shule? Muda je wa kukaa nao? Elimu yake ameipatia wapi? Kwenye familia aliyotoka je? Wazazi wake wapo? Na je wanajivunia yeye kwa kiasi gani?
Sasa ili kupata majibu ya maswali hayo yote ilibidi tumtafute Bi Brenda Msangi-Kinemo ambaye ndo nilikua namzungumzia hapo juu. Kama wewe utakua mtu wa kujua ambayo yanaendelea nchini, na pia kama ni mkazi wa Dar es Salaam basi lazima utakua unajua kuhusu hospitali ya CCBRT ambayo kwa kiasi kikubwa imesaidia na inaendelea kutoa huduma za macho, mifupa na magonjwa mengine kwa watu wengi kwenye nchi yetu. Sasa Bi Brenda yeye ndo Mkurugenzi pale. Na amekua kwenye cheo hicho kwa zaidi ya miaka minne sasa na hiyo ukiachilia mbali miaka ambayo alikua akifanya kazi pale wakati bado hakua Mkurugenzi.
Yeye ni mtaalamu wa masuala ya afya, hicho ndo ambacho aliendea skuli huko nchini Uingereza na kwa mujibu wa baadhi ya majarida ambayo nimesoma maisha yake kama yalikua yanataka kubaki huko baada ya kuhutimu ila aliporudi nyumbani na kupata nafasi pale hospitali mambo mengi yalibadilika. Kwenye kipindi hiki anatusimulia jinsi ambavyo hayo yalitokea. Na aina ya maamuzi ambayo ilibidi ayachukue ili mambo yatuwame.
Kwa wasichana wengi hasa wale ambao wanakua na kuanza kujitafuta Brenda ni role model wao sana na ni nafasi ambayo kwake yeye ilikuja baada ya kuwa anaandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuhusu kupambana na kuweza kuvaa kofia zaidi ya moja kwenye maisha ukiwa kama mwanamke. Humu pia ananiambia jinsi ambavyo hizo nondo za ku inspire zilivyoanza, ananiambia jinsi ambavyo alikua akisoma na kufanya kazi na wakati mwengine jinsi ambavyo majukumu yalikua yakimzidi mpaka anakaribia kukata tamaa ila msukumo ambao alikua akiupata kutoka ndani yake ndo ambao ulimfikisha alipo. Aliamini kwamba kuna wanawake na wasichana wengi ambao wanapitia kwenye mitihani ambayo yeye alikua nayo na kama yeye aliweza kushinda basi aliona atumie sauti yake na busara zake kuwaambia wengine kama hakuna kinacho shindikana kama nia inakuwepo.
Binafsi nilijichotea mengi sana kutoka kwenye kisima chake cha busara na uthubutu na bado darasa naendelea kulipata kwasababu nafuatilia yale anayo yafanya na ambayo anayaandika ili kusaidia wengine wasijione wako peke yao.
Mungu amueke na aendelee kumsimamia kwenye kazi zake na maono yake ambayo yanasaidia watu wengi wengine kuanzia ofisini kwake mpaka kanisani na nyumbani.
Yangu matumaini nawe uta enjoy na kupata faida kwenye episode hii kama ilivyo nia yetu.
Love,
Salama.
--- Support this podcast: https://podcasters.spotify.com/pod/show/yahstonetown/supportWeitere Episoden von „Salama Na“
Verpasse keine Episode von “Salama Na” und abonniere ihn in der kostenlosen GetPodcast App.