Salama Na podcast

SE7EP36 - SALAMA NA ALLY BEE | KULE NI KULE…

16.2.2023
0:00
1:04:32
15 Sekunden vorwärts
15 Sekunden vorwärts

Kwenye jiji la ‘Maraha’ hapa nyumbani kwetu Tanzania ambayo kwa miaka ya hivi karibuni sehemu za starehe zimekua tele na kila mmoja ana uwezo wa kula bata zake vizuri tu kulingana na urefu wa mfuko wake basi hakuna ambaye HAJUI jina la DJ huyu mahiri ambaye kwa ubunifu wake ameweza sana kubadilisha kabisa jinsi ambavyo wenzake walomtangulia walikua wanafanya. Yaani Ally alikichukua kitabu cha jinsi ya kutoa burudani kama DJ na kukichanachana na kisha akaanza kuandika cha kwake, ambacho mpaka tunaenda mtamboni kiiila msomaji wake anapeeenda ambayo yameandikwa na ambayo anaendelea kuyaandika.

Wakati msimu huu unaanza Ally Bee hakua moja ya majina ambayo yalikua yameandikwa kama mmoja ya watu ambao tungependa kujua story ya maisha yake, kutaka kujua nini kinampa hamasa ya kufanya ambacho anafanya na pengine mambo mengine tele ambayo atakua na uhuru wa ku share na sisi. Ila kuna siku nilikua nyumbani na Rafiki yangu ambaye pia ni mdogo wangu Ndugu Sadam Almando Sanare ambaye nilikua namuuliza maswali kuhusu Dj mwengine kabisa huku nikilalamika kuhusu huyo mtu kwamba pengine kuna jambo haliko sawa kuhusu simulizi zake za baadhi ya mambo maana amekua kama anaongelea sana skuizi, then yeye akaniambia kuhusu Ally Bee (binafsi hupenda kumuita Ally Bee kwasababu wote tunamjua nyuki, na ukali wake lakini asali yake sote ndo kama hivyo, hopefully it will make sense kwake someday 😄). So wakati ananiambia nami tayari nilikua nishamuona, basi mengine yakaendelea kwenye meza yetu adhimu.

Story ya maisha yake Ndugu yetu huyu ni ya mateso mengi sana, ila kwa sasa na hata pengine mwanzo kwa adha zote hizo tunamshukuru Allah kwa hayo yote maana hayo ndo yameleta hasira za yeye kutaka zaidi, kuomba zaidi na kufanyia kazi zaidi yote ambayo anayo leo. Ally anakumbuka jinsi alivyofika Dar es Salaam mara ya kwanza na pia amenihadithia adha ya kutokua na sehemu ya kukaa hasa unapokua umekuja mjini mara ya kwanza. Alinifanya nijiulize maswali mengi sana mimi kama binadamu wa kawaida kabisa, au ambaye Mwenyezi kanibariki kwa mengi zaidi ya wengine, nini nafanya kuwasaidia ambao nawaona barabarani? Au ambao hawana uwezo wa kunifikia lakini wana uhitaji? Kanifundisha kuhusu kutochukulia maisha au nafasi ambazo tunazo kwenye maisha yetu kwamba ni kawaida tu. Ki ukweli kila ambacho tunacho kwenye maisha yetu TUNA KILA SABABU YA KUMSHUKURU AMBAYE AMETUPA. Ila pia inabidi mara moja moja tujipigie makofi kwa mbali ambapo tumetoka na ambapo tumefika lakini zaidi tumuombe Mwenyezi Mungu azidi kutuimarisha na kutufungulia milango ya Kheri, ZAIDI.

Niamini mimi nikikuambia kuhusu kutoa, kwamba kutoa ni raha zaidi kuliko kupokea ingawa wengi wetu tunapenda zaidi kupokea, ukitaka kujua hilo jaribu kwa kuanza kumpa hata mtu zawadi ndogo tu, hata pipi ambayo alikua hategemei kama utampa au utakumbuka, sura yake itakueleza mengi hata kama yeye ataamua asikuambie kwasababu zake zozote tu. Ally alisaidiwa na mtu ambaye hata walikua hawafahamiani na kuamua kumpa hifadhi katika sehemu ambayo yeye alikua anakaa. Pengine yeye alipofanya wala hakujua kama Ndugu Ally atakuja kuwa mmoja wa ma DJ HODARI na Hyper Man bora ambae nchi hii imewahi kuona.

Leo ningependa tujifunze kuhusu hilo, kuhusu kuwa kind, kuhusu kuwapa watu nafasi kwenye maisha yetu na kutosubiri malipo kutoka kwao maana pengine yanaweza yasije lakini wewe tayari unakua ushamaliza kazi yako.

Yangu matumaini story ya DJ Ally Bee itakua na impact kwenye maisha yako kama ambavyo imekua kwenye maisha yangu.

Enjoy and stay BLESSED.

Love,

Salama.

Weitere Episoden von „Salama Na“