Salama Na podcast

SE7EP33 - SALAMA NA MR BLUE | KHERI

1/26/2023
0:00
56:32
Rewind 15 seconds
Fast Forward 15 seconds
Kheri Sameer aka Mr Blue aka Lil Sama aka Bayser ni mdogo wangu, mdogo wangu kabisa na uzuri nakumbuka kabisa mara ya kwanza kuonana nae na mpaka alivyokua amevaa. Jezi ya Denver Nuggets, jeans ya light blue na sneakers nyeupeeehh na chain ya Silver, kwenye maskio alikua na hereni za kung’ara zile ambazo zilikua si za kitoboa skio, zilikua zina smaku na nazijua zaidi kwasababu Marehemu cousin brother wangu alikua nazo maana nyumbani ilikua hairuhusiwi kutoboa maskio enzi hizo. Alikua msafi, ana swagg ya kuongea na hata jinsi alivyokua anajibeba. Alikua wa moto sana unaweza kusema hivyo, au niseme hivyo. Kila ‘mtoto’ na kijana alitamani kuwa kama yeye kwa kila kitu, muonekano mpaka hit songs kwenye radio na TV. Blue alikua na mtu ambaye anamsimamia na huyo hakua mwengine bali G Lover, meneja na Dj ambaye alikua anasimamia kazi zake yeye pamoja na wasanii wengine kama Ally Kiba, Ally Com na Abby Skills kwa kuwataja kwa uchache na wasanii wake hao wote walikua wa moooto sana. Ngoma kali, video mbaya, show nyingi na kwa ‘mhindi’ wanauza sana. Na kuanzia hapo kwa mhindi na kuuza sana ndo ambapo kuliweza kuwapoteza wengi kwasababu wengi walikua wadogo sana na pesa ilikua nyingi. Fitna na utovu wa nidhamu wa kupindukia ulianzia hapo. Wakati naandika hii nilimuwaza Ally Kiba na jinsi ambavyo ameweza ku maintain class flani toka siku ya kwanza tunamskia na mpaka leo regardless ya mengi ambayo yametokea hapo katikati, HAKUWAHI KUPOTEA. Kwa hilo naamini anastahili HESHIMA na recognition ya hali ya juu pengine kuliko tunayompa maana dah, mambo yalikua mengi sana enzi hizo. Kuna usemi kwamba wakati ni mwalimu mzuri sana na kwa uelewa wangu hakuna ambaye anaweza kuelezea experience kama ilivyo elezewa kwenye usemi huo. Wakati ndo ambao unatufunza na kutuonyesha vitu na watu wengi, ambao tulikua tukiwaamini na wengine kuto kuwaamini, kuwapenda na wengine kuto wapenda, kudhani unajua na ki ukweli hujui, kudhania umezama kwenye dimbwi na mapenzi na huyo alo nae ndo wako wa milele na kumbe si hivyo na hayo yote unayaelewa within kipindi fulani, miaka inavyokwenda ndo na wewe unaelewa na kujifunza mambo kwa uwezo na uelewa wako. Moment za ‘anha’ na ‘wow’ huwa nyingi sana. Wakati ni MWALIMU na majuto huwa ni mjukuu, nadhani utakua umenielewa. Mr Blue alikua na dunia kwenye miguu yake, ilikua yeye tu aseme anatakaje na anataka ielekee wapi na hivyo ndo ingekua ila haikua hivyo ndo jambo la kusikitisha lakini bahati kubwa ambayo mwenzetu alikua nayo au yuko nayo ni kwamba hayo yote yalitokea mapema sana, wakati yuko mdogo sana kwenye dunia ambayo wengi walikua wakimuangalia na kumpenda sana. Yeye baada ya kuona mapenzi na shangwe hilo basi akadata na akaanza kuwa mgumu kufanya nae kazi, akawa na marafiki tele ambao hakua anawajua kabla hajawa Lil Sama na baadae Mr Blue. Akawa hasikii la muadhini wala mnadi sala. Akajiingiza kwenye uvutaji wa bangi isokua na staha, akaondoka nyumbani na kwenda kuishi kwenye ma ghetto na wana wasokua na ramani. Akawa ana party Jumatatu mpaka Jumatatu. Studio haonekani, kwenye interview hatokei na wale watangazaji ambao walikua wanapiga mgoma zake kwenye Radio akawa hata salaam hawapi. Producer na meneja nao wakagombana nae kwasababu sitofahamu ya pesa kwa mhindi ilishika hatamu. Mwanzo nilisema Blue ana Kheri sana kama jina lake kwasababu hayo yote yalitokea wakati mdogo sana, dunia ilimfunza nae akafundishika, wakati dunia hiyo ikiwa inamfunza alikua mwanafunzi mzuri sana kwasababu darasa alilolipata wakati kakata ringi ndo ambalo limefanya awe BORA na ajitambue LEO HII. Kwenye meza yetu ya kigae na kiti chakavu Blue ananielezea hustle zote ambazo alishawahi kuzipitia wakati anakua na huku akiwa anajitafuta na kwa uelewa wangu itasaidia wengi ambao wanaaza au wataanza kuzishika pesa mapema au hata ambao watapata mafanikio huko mbeleni watajua jinsi ya ‘kujibeba’ kutokana na maongezi yetu haya. Maongezi haya yalikua yafanyike mapema tu lakini u busy wa Lil Sama na kupishana kwa ratiba zetu ndo kulifanya yatokee --- Support this podcast: https://podcasters.spotify.com/pod/show/yahstonetown/support

More episodes from "Salama Na"