Salama Na podcast

SE7EP31 - SALAMA NA KUSAH | NG’WANA AZAIZA!!

1/12/2023
0:00
50:38
Rewind 15 seconds
Fast Forward 15 seconds

Kutoka zake Lushoto huku mkoani Tanga ni kijana mtanashati ambaye anajua kama amekuja town au jijini Dar es Salaam kwasababu ya kusaka pesa ili abadilishe maisha yake na ya wale ambao wamemzunguka. Na kila alikumbuka ambapo ametoka basi spidi ya kuhakikisha kalamu yake haivuji na inaandika kwa muandiko mzuri ili kila ambaye atabahatika kusoma kile ambacho yeye kakiwaza na kukiandika basi azame kwenye dimbwi lake na endelee kumsikiliza mpaka pale yeye mambo yake yatakapoenda, na kwa story ambazo amenipa basi ukinasa kwenye kitabu chake itakuia vigumu kutoka kwasababu amepanga kuwepo kwa muda mrefu sana, nia na madhumuni yake ni kuhakikisha yupo yupo sana.

Kusah ananihadithia aina ya kazi ambazo ilibidi afanye wakati anakua, ilikua inabidi aende shuleni ila pia amsaidie Bi Mkubwa wake ambaye alikua anafanya kazi nyingi kuhakikisha watoto wanakula na kusoma, ikiwa pamoja na kuuza pombe za kienyeji ambazo ni haramu. Uvunjaji huo wa sheria ulikua unaifanya familia iingie matatani na anakumbuka kipindi ambacho ilikua inabidi amsaidie Mama kuficha vitendea kazi na vithibiti pale msako wa ghafla unapotokea. Kama mtoto wa kiume kwa utashi wake tu toka akiwa na umri mdogo aliona huo ulikua ni wajibu wake kuhakikisha Mama yake yuko Salama.

Tukizungumzia suala zima la kazi ambayo ameichagua kufanya sasa yeye ni fundi, moja ya mafundi hodari ambao ameshaanza kujijengea na fan base yake nzuri tu, show za ndani na nje anafanya na anaelewa jinsi ya kuji brand na nini cha kufanya wakati gani na kitamfaaje. Mambo ambayo anayafanya na kuyafanikisha ni ambayo yawewachukua baadhi ya watu muda kuweza kuyakamilisha lakini yeye kwa kipindi kifupi ameweza kupiga hatua kubwa na pengine ingekua kubwa zaidi kama kusingekua na kuchelewa flani hivi ambako kulitokea baada kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Ruby ambao kwa taarifa tulizokua tunazisikia na nyengine kuzisoma mtandaoni mahusiono yao hayakua mazuri kwa afya ya kila mmoja wao.

Kusah anazungumza nasi kuhusu hilo, kuhusu Mama yake, kuhusu Lushoto na plan ya maisha yake. Ameongea na sisi kuhusu kazi alizowahi kufanya maishani mwake, jinsi alivyoweza kutoka kwenye ‘toxic’ relationship ambayo ilikua ikimuumiza yeye na aliyekua partner wake. Pia anatuhadithia suala la yeye kuwa Baba kwa mara ya kwanza na mara ya pili. Tumeongelea pia mahusiano yake na Aunt Ezekiel na plan zake za huko mbele akiwa kama mwanamuziki ambaye amejikita zaidi.

Yangu matumaini uta enjoy kila sekunde ya maongezi yetu haya na mawili matatu utayapata ya kukufunza jambo.

Tafadhali enjoy.

Love,

Salama.

More episodes from "Salama Na"