Salama Na podcast

Ep. 54 - Salama Na VANNY BOY | NDAGHA

0:00
1:14:32
Rewind 15 seconds
Fast Forward 15 seconds

Kutoka kwao Mbeya mpaka Dar es Salaam kwaajili ya kutafuta maisha bora na maendeleo kama wengi wetu ndo ilikua nia na madhumuni ya Raymond wa enzi hizo. Ingawa kuna kipindi ilifika alikua hataki kabisa kuskia habari za muziki, ila alipoambia kama kuna pesa ndani yake katika huo mchongo wa mashindano ambayo aliitiwa na akiangalia nyumbani moja haikai na mbili haijulikani ilipo akaona basi sawa, kwani nini? Na huo ndo ulikua mwanzo wa safari nzuri ya ki superstar ambayo anaishi nayo sasa.

Najua wengi wenu mlikua mnadhani labda yangezungumziwa madhila alokua nayo sasa ila kwa bahati mbaya (kwako) na nzuri kwetu, sisi tulizungumza naye kabla. So hii ilikua free na natural kama ambayo utaiona au kuiskiliza. Wengi wetu huwa tunapitia madhila na mitihani mingi tu kabla ya kujielewa na kusimama sawa sawa, na kupitia hayo ndo kujifunza na kuwa BORA kunatokea. Kuna msemo mmoja wa Kiswahili unaoenda kama, ‘asipo chafuka, atajifunzaje’, something like that.

Mimi Ray huyu nilianza kumsikia vizuri zaidi kutoka kwa AY ambaye ali spend naye muda mwingi hapa Bongo wakati wanafanya rekodi remix ya Zigo na nchini Afrika ya Kusini wakati Zee ameenda ku shoot video ya wimbo huo ambao Diamond Platnumz ndo ameshirikishwa, ila Vanny Boy alikuwepo all the way na mpaka kwenye video akatokea. AY aliniambia kuhusu ucheshi wake na uhodari wake, na uhodari huo ameuzungumza humu kwenye maongezi yetu mimi na yeye. Aliniambia jinsi ambavyo alikua akitumia kipaji chake enzi hizo kwa kuwaandikia wenzake wimbo mmoja na pengine mpaka album kwa shilingi ELFU THELATHINI TU.

Njia ambazo watu wengi wamepita haiwezi kuwa ndo njia ambayo kila mmoja wetu atapitia pia, ila kunaweza kuwa na mifanano ya hapa na pale, na hii ndo nia na madhumuni ya kipindi hiki. Tunataka wewe usikie na ujifunze ili ujue ‘unatokaje’ au watu walipenya vipi mpaka wakafika!

Sasa ni mmoja ya wasanii wakubwa tu hapa barani Afrika na duniani anafahamika. Bango la album yake linaning’inia kwenye mitaa ya Times Square huko NY City kwenye mji ambao raia wa nchi mbalimbali duniani wanaishi na kupitia. Sidhani kama wakati anahangaikia kufua nguo zake zilizomwagikiwa mafuta ya mawese wakati akiwa safarini kwenye lori kutoka Mbeya kuja Dar aliwahi kuwaza jambo kama hilo.

Mimi na yeye tulizungumzia pia mahusiano yake na wazazi wake, familia ya kufikia ya Baba yake ambaye aliachana na Mama yake na kuhamia na mtu mwengine si mbali na wao walipokua wanakaa. Tumeongelea mapenzi yake na muziki na kipaji chake cha uandishi. Tumeongelea jinsi ambavyo Madee alimpokea na Babu Tale ambavyo alikua na kama kusita hivi kwenye suala la yeye kusajiliwa WCB na mambo mengine mengi ya maisha. Yangu matumaini kama ilivyo ada, hapa utajifunza jambo pia.

Tafadhali enjoy.

Love,

Salama.

--- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

More episodes from "Salama Na"

 • Salama Na podcast

  Ep. 55 - Salama Na PROFESA | MAPINDUZI HALISI

  1:27:20

  SALAMA NA PROF JAY --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support
 • Salama Na podcast

  Ep. 54 - Salama Na VANNY BOY | NDAGHA

  1:14:32

  Kutoka kwao Mbeya mpaka Dar es Salaam kwaajili ya kutafuta maisha bora na maendeleo kama wengi wetu ndo ilikua nia na madhumuni ya Raymond wa enzi hizo. Ingawa kuna kipindi ilifika alikua hataki kabisa kuskia habari za muziki, ila alipoambia kama kuna pesa ndani yake katika huo mchongo wa mashindano ambayo aliitiwa na akiangalia nyumbani moja haikai na mbili haijulikani ilipo akaona basi sawa, kwani nini? Na huo ndo ulikua mwanzo wa safari nzuri ya ki superstar ambayo anaishi nayo sasa. Najua wengi wenu mlikua mnadhani labda yangezungumziwa madhila alokua nayo sasa ila kwa bahati mbaya (kwako) na nzuri kwetu, sisi tulizungumza naye kabla. So hii ilikua free na natural kama ambayo utaiona au kuiskiliza. Wengi wetu huwa tunapitia madhila na mitihani mingi tu kabla ya kujielewa na kusimama sawa sawa, na kupitia hayo ndo kujifunza na kuwa BORA kunatokea. Kuna msemo mmoja wa Kiswahili unaoenda kama, ‘asipo chafuka, atajifunzaje’, something like that. Mimi Ray huyu nilianza kumsikia vizuri zaidi kutoka kwa AY ambaye ali spend naye muda mwingi hapa Bongo wakati wanafanya rekodi remix ya Zigo na nchini Afrika ya Kusini wakati Zee ameenda ku shoot video ya wimbo huo ambao Diamond Platnumz ndo ameshirikishwa, ila Vanny Boy alikuwepo all the way na mpaka kwenye video akatokea. AY aliniambia kuhusu ucheshi wake na uhodari wake, na uhodari huo ameuzungumza humu kwenye maongezi yetu mimi na yeye. Aliniambia jinsi ambavyo alikua akitumia kipaji chake enzi hizo kwa kuwaandikia wenzake wimbo mmoja na pengine mpaka album kwa shilingi ELFU THELATHINI TU. Njia ambazo watu wengi wamepita haiwezi kuwa ndo njia ambayo kila mmoja wetu atapitia pia, ila kunaweza kuwa na mifanano ya hapa na pale, na hii ndo nia na madhumuni ya kipindi hiki. Tunataka wewe usikie na ujifunze ili ujue ‘unatokaje’ au watu walipenya vipi mpaka wakafika! Sasa ni mmoja ya wasanii wakubwa tu hapa barani Afrika na duniani anafahamika. Bango la album yake linaning’inia kwenye mitaa ya Times Square huko NY City kwenye mji ambao raia wa nchi mbalimbali duniani wanaishi na kupitia. Sidhani kama wakati anahangaikia kufua nguo zake zilizomwagikiwa mafuta ya mawese wakati akiwa safarini kwenye lori kutoka Mbeya kuja Dar aliwahi kuwaza jambo kama hilo. Mimi na yeye tulizungumzia pia mahusiano yake na wazazi wake, familia ya kufikia ya Baba yake ambaye aliachana na Mama yake na kuhamia na mtu mwengine si mbali na wao walipokua wanakaa. Tumeongelea mapenzi yake na muziki na kipaji chake cha uandishi. Tumeongelea jinsi ambavyo Madee alimpokea na Babu Tale ambavyo alikua na kama kusita hivi kwenye suala la yeye kusajiliwa WCB na mambo mengine mengi ya maisha. Yangu matumaini kama ilivyo ada, hapa utajifunza jambo pia. Tafadhali enjoy. Love, Salama. --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support
 • Salama Na podcast

  Don't miss an episode of Salama Na and subscribe to it in the GetPodcast app.

  iOS buttonAndroid button
 • Salama Na podcast

  Ep. 53 - Salama Na NANDY | MNOGESHAJI

  1:04:04

  Huyu si moja ya marafiki zangu, as in si Mtu amable nafahamiana naye sana, ambaye nishawahi kukaa naye muda mrefu na kupiga story, au kusafiri naye au kuwa studio wakati anafanya mambo yake au namjua mzazi wake au mtu wake wa karibu kwenye familia yake ila nawajua watu ambao wanamfahamu kwa ukaribu na watu hao ndo ambao walinipa mimi mawazo ya kutaka kumfahamu vizuri binti huyu hodari wa ki Tanzania bila ya hata ya wao kujua. Baadhi ya Dada zangu walifahamiana naye kwenye kipindi cha msiba wa Marehemu Ruge Mutahaba, kipindi hiko kilikua cha masikitiko kwao na kwake pia. Nandy alikua na ukaribu mwingi na Ruge, alishawahi kumtembelea hospitali mara kadhaa na pia alikua na mawasiliano ya moja kwa moja na watu wa karibu wa familia kipindi kile ambacho Ruge alikua hana tena mawasiliano naye moja kwa moja. Siku ambayo Ruge alitangulia muelle ya haki, muda si mrefu kabla ya hilo halijatokea Nandy ananiambia alizungumza na nesi wa zamu siku hiyo na pia alimuekea simu kwa ukaribu na alimsikia akiwa anapumua. Wapi alikua wakati anapata habari hii iko kwenye maongezi yetu haya, humu pia utaelewa connection ambayo sisi binadamu tunayo na watu ambao tunawapenda na wanao wanatupenda. Najua siku hazigandi kama ambavyo Lady Jd alishawahi kuimba na ndo  nikawaza, hivi ushawahi kuwaza Nandy amekua kiasi gani toka msiba wa Ruge utokee? Unakumbuka baadhi ya maneno yalosemwa juu ya career yake baada ya msiba ule? Tunafahamu kwamba alipoteza rafiki, mentor, baba na kama tochi yake? Mimi huwaza haya sana, na hilo la yeye kujidhatiti na kukaza mwendo ndo ambalo lilifanya mimi binafsi niseme you know what, it’s time. Nandy ni MPAMBANAJI, anaupenda muziki na kama mtu mwengine yoyote mwenye jitihada basi Mungu humfungulia milango ya Kheri. Kaniambia humu kwenye mangezi yetu kwamba safari yake ya kwanza kwenda nchini Nigeria kwenye mashindano ya kuimba alimuambia Mama yake wakati yumo ndani ya ndege, alipomaliza hutuba yake fupi alizima simu na wheels up, to Lagos ambako alihakikisha anapigana mpaka fainali na kumaliza nafasi ya tatu. Si kitu kidogo kwa binti ambaye aliamua kuweka shule pembeni ili atimize ndoto yake, ndoto ambayo hata Mama yake mzazi hakua na taarifa nayo. Siku zinakwenda, maisha yanasonga na yeye ameendelea kukimbiza ndoto yake na mpaka tunaenda mitamboni, Nandy ni mmoja wa wasanii wa kike wakubwa sana hapa nyumbani na barani Afrika na hata Ulaya na Marekani na ukitizama vizuri utajua kwamba huu ni mwanzo tu wa mazuri ambayo yatatokea katika maisha yake. Mimi na yeye tulizungumzia mahusiano hayo pamoja na kukimbiza ndoto zetu. Tuliongelea Bill Nas na kiwanda cha muziki wa Bongo Flava. Tuliongelea muziki wake na collabo ambazo amewahi kufanya. Hapo hapo nilitaka kujua pia yeye ni mtu wa aina gani na ni vitu gani vinamsukuma kutaka atake zaidi na sehemu ambayo anajiona huko mbeleni In Shaa Allah. Yangu matumaini kama kawaida ni kwamba utajifunza mawili matatu ambayo yatakusaidia kupambana na mitihani ya maisha kwasababu tu umejifunza kutokana na sehemu wenzetu hupitia kwenye maisha yao. Tafadhali Enjoy. Love, Salama. --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support
 • Salama Na podcast

  Ep. 52 - Salama Na HAJI | ALIYE KUTWIKA NDIYE ATAKAYEKUTUA

  1:23:44

  Haji Sunday Manara nlitaka kusema ni rafiki YANGU ila vacati navaza hilo nikakumbuka mmh, Haji Sunday Manara ni rafiki wa WATU WENGI hususan mashabiki wa klabu wangu pendwa na zaidi kwa watu ambao hawapendi hata mpira ila wanampenda tu jinsi anavyoseti mambo yake na anavyoigeuza sehemu yoyote aendayo kama sehemu yake ya kujitamba na kujitutumua na tofauti yake na WACHACHE ambao wanafanya kazi kama yake ni kwamba yeye anaweza KUYATEMBEA yale anayo YAONGEA. Mapenzi yangu kwake ni ya first class na namini hata yeye analifahamu hilo, huwa namtazama kwa kuvutiwa hasa kwababu ya anavyojibeba na kukiaminisha kile ambacho anakisema, iwe kuhusu Simba, bidhaa ambayo anaitangaza au hata simulizi za maisha , vyovyote vile vitakufanya utake kumskiliza kwa umakini, na pia ni lazima ucheke. Utashi wake kwenye mambo mengi pia ni jambo la kupendeza, ukiniuliza mimi nitakuambia sawa, hata kama ni mtoto wa Kariakoo, ni watoto wa Kariakoo wangapi ambao wewe unawajua wana kipaji cha kuongea na kumfanya mtu ajiskie kama ambavyo Haji anafanya baadhi ya watu wajiskie? Iwe kwa kuzodoa au kusifia wangapi? Maneno ya papo kwa papo au hata ya kujindaa (hapo ndo utachoka kabisa), yupi? Urafiki wetu ulianzia pale kwenye USIMBA DAMU na tuli click tu moja kwa moja, niliamini timu wangu ido kwenye mikono salama kabisa kama jina langu, tufungwe atasema maneno ya kutufanya tunyoshe mgongo na kusimama vuzuri na tukishinda well tukishinda mziki unaufahamu vizuri tu, na tukisajili je? Ahaha… Huyu mtu huya ananipa raha sana, Nba hiyo neo ilikua sababu ya Mimi na wenzangu kumvuta kitini. Maneno mengi yamekua yakisemwa juu yake na pia mdomo wake huo ulishawahi kumtia matatani kipindi flani kile ambacho Bwana Mo Dewji alipopata matataizo, si unakumbuka? Haji alitiwa ndani siku kadhaa mpaka alipokuja kuwa cleared kwamba hakua anahusika, sikuongea nae kuhusu hilo kwasababu tu za kutotaka asiwe comfy kwenye kiti chetu ( ingawa najua ningeuliza asingekua na hiyana hata). Maneno mengine ni kuhusu urafiki wake na matajiri wa mjini ambao wengine ni wamiliki wa time pinzani za muajiri wake, hili likoje? Huwa anasumbuka wananchi wanapolileta kwenye comments za ukurasa wake maarufu wa Intagram? Mzaliwa wa Udachini kule nchini Holland, Haji amekua hapa Dar es Salaam kwa malezi ya Bibi na Babu zake maana kipindi hicho Mzee wake alikua anakipiga nje zaidi, mimi nilitaka kujua hiyo historia yake na mpira na Mzee wake, Yanga (ambayo tunaweza kusema ni team ya familia), elimu yake na mambo ya ndoa na scandal za mitandaoni za hapa na pale. Pia tuliongelea pale alipokua wakati shabiki wa Simba Bwana Hamisi Kingwangalla alipohoji uwekezaji wa Mo Dewji na bilioni 20 za uwekezaji, na mano yake hasa kuhusu hiyo situation. Nimecheka sana, nimeskiliza sana, nime admire sana na zaidi nimejifunza mengi ambayo nilikua siyafahamu kuhusu mtu huyo maalum na tunu ya Taifa hili. Yangu matumani utaelewa na kujifunza jambo hapa. Tafadhaki enjoy rafiki. Love, Salama. --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support
 • Salama Na podcast

  Ep. 51 - Salama Na Babu Tale | JUGGLER

  1:16:40

  Hamis Tale Tale ni MWAMBA wa maisha yake na ya wale walomzunguka kwa miaka nenda miaka rudi na kutoka upande huu wa muandishi na mtangazaji ni heshima tu kwenda mbele. Kuna msemo mmoja wa Kiswahili kuhusu nyani ambaye unamkuta mjini. Ya kwamba anakua kashakwepa MISHALE ya kutosha kwahiyo unapomkuta town inabidi umpe heshima zake za kutosha. Kwa waasisi wa Bongo Flava jina lake kuwa juu pale na haiwezi kuwa kosa hata kidogo na kuna wasanii kibao ambao wana mshutumu kwa mambo mengi lakini kuna wale ambao hawawezi kumsahau maishani mwao kwa sababu ya mchango mkubwa ambao amewapa. Na vile vile ukimtaka mtu wa kukuelezea tabia na uzuri wa watu wa iaina zote katika industry hii basi Babu Tale ndo ambaye atakuelezea hilo kwa kinaga ubaga maana akiachana na ucheshi wake, Tale pia ni msimuliaji habari mzuri tu. So kuanzia kwa Marehemu Kaka yake Abdu Bonge mpaka kwa huyu anayevaa kaunda suti zilizonyooka ndo sisi tulipopataka, ametoka umbali gani? Haya yote aliyonayo ilikua ndo mipango yake? Ki ukweli mmoja kama anaamini ya kuwa kuna yatu wanakua wamekaa tu wanaangalia progress zeta kwa mbali na kuona haswa umbali gani watu wametembea mpaka kufika kwa mfano ambapo Tale amefika basi bila ya shaka atakua ametia nne yake huku akiwa kapendeza sana na kumpigia makofi tu kwa yale aliyoweza kuyafikia mpaka sasa. Ukichukulia huyu ni Kijana ambaye kuna wakati flani katika maisha yake ilikua inabidi asubiriane na mmoja ya ndugu zake ili waweze kubadilishana aidha viatu au uniform ili na yeye aweze kwenda shule! Nimekutana na watu wengi  katika maisha yangu na Tale yeye yake tabia ni kutokua na breki pale anapokua na lake, yale mambo ya sijui kulainisha maneno ili pengine asikuumize hisia zako yeye hana, kinda like me, la kusemwa lisemwe kisha maisha yaendelee, na hiyo ni kwa kumtakia mtu mema tu, pia anachekesha na anapenda kucheka pia, also… Mkali, sio wa ‘kulealea’, sio babysitter hata kidogo na hiyo yote ni kwa kutaka JEMA kwa mtu ambaye anamsimamia. Najua kama binadamu atakua na mapungufu yake na hayo ndo yako pia kwenye maneno ya baadhi ya wasanii ambao ameshawahi kufanya nao kazi. Tale ana khadithi ya kila mmoja wetu kwenye kiwanda hiki cha muziki na burudani na nna uhakika miaka kadhaa ya mbele atakua na khadithi za wanasiasa wenzake na viongozi ambao kuanzika mwaka huu anaanza kuwa nao kwa muda mrefu kwenye maisha yake. Mwaka jana Babu Tale alimpoteza mke wake kipenzi ambaye alitangulia mbele ya haki na kumuachia watoto ambao sasa yeye ndo anaye waangalia kwa msaada pia wa baadhi ya ndugu zake. Hii ilikua habari nzito kwa kila mtu, mke wake amble wengi tulikua tunamfahamu zaidi kupitia mitandano ya kijamii, mimi nishawahi kukutana naye mara kadhaa, alikua Mrembo sana wa sura na roho, Mwenyezi Mungu Amrehemu. Mengi sana yalisemwa na kwa ufahamu wangu nikaona basi hakuna wa kutuambia ambayo tunadhani tuna haki ya kuyajua zaidi yake YEYE. Nini haswa kilitokea? Natumai maongezi yetu haya yatakupa somo flani kwa mambo kadhaa ambayo tunakutana nayo maishani mwetu, Tale amanitajia watu ambao kwa kiasi kikubwa wanamsaidia kumpa faraja baada ya mkewe kutangulia mbele ya haki, na watu hao hata sio NDUGU ZAKE, ingawa najua nao kwa kiasi chao wanamsaidia ki vyao. Hili kwangu liliingia haswa. Humu kuna mengi tuliyagusia na hakua na hiyana kutuambia mawazo yake na kwa hilo napenda kumshukuru. Tafadhali enjoy session hii ambayo kama kawaida natumai itakufunza mambo mawili matatu, iwe kuhusu mapenzi, maisha, kazi, watoto, muziki, marafiki na hata siasa, Na pengene hata jinsi ya kukimbiza naoto zako! Love, Salama --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support
 • Salama Na podcast

  Ep. 50 - Salama Na SUGU | UJIO WA UMRI

  1:10:30

  Turudi nyuma mwaka 1999 wakati nilipomaliza kidato cha nne kwahiyo nilikua sina mitkasi mingi zaidi ya kumkimbia Mama inapofika mchana ili niende kucheza zangu basketball pale Msasani kiwanja cha Pazi. Nlikua natokea zangu Mbagala Charambe nachukua zangu basi mappa Mbagala Rangi tatu then muunganisho unaendelea mpaka nafika zangu mazoezini, nilifanya urafiki na makonda na madereva weeengi kiasi kwamba nilikua ‘staff’ kwenye daladala nyingi, na huwezi kuamini nyingi pia nilikua nikiingia basi radio nlikua namiliki MIMI. Station gani tunaskiliza au tape gani tunaweka ili safari inoge na muziki. Nakumbuka jinsi ambavyo Sugu alikua anaikosha, anakosha nafsi yangu na ya abiria wote ambao walikua wanasafiri nasi basi moja. Chini ya miaka 18 ilikua inaongea na mimi haswam inanifanya nisitake kuwa yule binti ambale Sugu alikua namuongelea ASILAN! Mikononi mwa Polisi… Album kali kama Nje ya Bongo, Millenium, Muziki na Maisha zilifuata na wakati hizi nyengine zinatoka nami tayari nilishaacha kumtia wasiwasi Mama yangu wa kurudi nyumbani usiku na kuwa DJ wa muda ndani ya Daladala za Mbagala Posta au Mbagala Kariakoo na kuweza kupata kazi yangu ya kwanza pale Times FM kabla sijajiunga na EA Radio na TV. Mapenzi yangu kwa Sugu na muziki wake yako wazi na naamini na yeye anajua maana huwa namuambia kila tunapokutana, pia napenda kuwa around na yeye maana confidence yake ni kitu cha kujifunza. Haogopi, anajiamini na uthubutu wake katika mambo yake mengi ni jambo ambalo wengi wetu tunajifunza sana kutoka kwake. Kuanzia jinsi alivyokua anajibeba, mapinduzi ya uandishi na muziki ambayo amefanya na anaendelea kufanya mpaka leo hii ni kitu ambacho kama utakua unamfuatilia kwa karibu basi utakua huna la kufanya zaidi ya kupenda jinsi anavyofanya mambo yake. Siku zote nimekua nikitaka saaana kufanya nae interview lakini kama tujuavyo, Mungu ndo mpangaji wa yote na round hii ilikua ndo wakati muafaka. Nilimcheki naye akakiambia kwamba Mimi ni mtu pekee ambaye angependa aongee naye so mengine yakawa historia tu. Brother alikuja Dar es Salaam malum kabisa kwaajili ya kuongea na sisi na kwa hilo tunamshkuru sana. Mambo ya kisiasa yalikua sio focus yetu hata kidogo na badala yake tulitaka kumfahamu yeye zaidi na pengine mmoja anaweza kujifunza kwa kufuatilia tu nyenendo zake kwenye mitandao. Kaka alishawahi kwenda jela, amempoteza Mama yake kipenzi pia muda si mrefu baada ya yeye kutoka. Sisi tuliongea naye kuhusu mapenzi yake na Mama yake kipenzi Desderia ambaye hata jina la hoteli yake ameipa jina la Mama yake. Nilitaka kujua ukaribu wao huo ulitokana na nini, jinsi ambavyo Mama alimpa support kipindi hicho ambacho muziki ulikua unaonekana kama uhuni tu. Maoni yake kwenye masuala mbali mbali na kuhusu urafiki na mafanikio. Pia nilitaka kujua historia yake ya muziki na njia alizowahi kupita. Mambo mengine ni kuhusu suala la yeye kuwa Baba na mapenzi kwa ujumla. Yangu matumaini una enjoy maongezi haya na Kaka mkubwa na pia confidence yake kwenye masala mbalimbali itakufanya pia ujibebe kuelekea mbele! Tafadhali enjoy. Love, Salama --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support
 • Salama Na podcast

  Ep. 49 - Salama Na MAVOKO | WINGMAN

  1:05:30

  Kwa muda mrefu nimekua nikitaka kuongea na Mavoko ila ratiba zetu zilikua hazijawahi kuwa sawa na hivyo tukawa tunapishana tu. Kama mimi sina program naye basi yeye atakua free, na mimi nikiwa free basi yeye atakua na mipango ya kutoa kazi mpya ambayo itanifanya ningoje ili viende pamoja, au atakua kasafiri, au mimi nitakua nishaset watu wengine, ilikua kama tunacheza kidali po ila katikati ya mwezi wa kumi na mbili hatimaye yakatimia. Hakuna doubt juu ya uwezo wake popote pale utakapoenda ingawa baada ya yeye kuamua kuondoka kwenye label ya WCB kulikua na mengi yalosemwa na kutendwa na baadhi ya mashabiki yalikua yanaweza kukuaminisha jambo na mpaka kufikia pengine ku doubt huo uwezo wake. Mambo mengi yalisemwa, ya kusikitisha, ndoa haikuvunjika vizuri ila ambacho nilikiona kwake ni ustaarabu wa hali ya juu, wa kuwaacha walimwengu waseme na kufanya watakayo huku yeye akiwa ame focus kwenye kipaji chake na kujipanga upya. Moto wa Mama Richard anaujua mziki mwingi, ana uwezo mkubwa wa kuimba na kuandika na kucheza pia, ila kabla hajaingia kwenye label alikua anajulikana tu, ila kumfahamu vizuri na kuthamini kipaji chake kulikuja baada ya yeye kushirikiana na mmoja kama si msanii bora zaidi kuwahi kutokea na kuipeperusha zaidi bendera ya Tanzania ndani ya Diamond Platnumz. Ushirikiano wao ulitupa ‘anthem’ kadhaa ambazo mpaka leo ukiziskiliza hazichuji. Ilikua kama team ya wenye vipaji pekee, kama ni mfuatiliaji wa mpira wa kikapu hii tunaweza kuifananisha na ile zile team mbili za Mashariki na Magharibi ambazo zinakusanya wachezaji wenye uwezo wahali ya juu. Saasa, ikawaje hasa mpaka akaona aachane na all star hiyo na kupeleka team yake uwanjani akiwa solo? Nini hasa kilifanya mpaka afikie maamuzi hayo? Kuna mtu  au kitu kilimshinikiza? Je yalikua maamuzi sahihi? Pia kuna masuala binafsi ya kifamilia na suala la yeye kutomfahamu Baba yake takati anakua, elimu yeke, ndugu zake, Mama yake na muziki ulichomfanyia katika maisha yake. Mavoko huyu ambaye mimi namfahamu nilikutana naye Kampala, Uganda kama maka saba iliyopita na mazungumzo yetu yalikua yanahusu kipaji chake na jinsi ambavyo nilikua naona ‘hapewi’ nafasi maana kama ngoma zake zilikua nzuri tu, video ndo usiseme ila hakuna na spotlight aliyokua anastahili, peleka mbele miaka mpaka 2021 ambapo alipata nafasi kwa miaka takriban miwili na nusu kufanya kazi na lebo bora zaidi ila baada ya muda akaamua kubwaga? Kwanini hasa? Sote tunajua kama nyasi za jirani huonekana zimestawi kweli kweli ila ukifika na kuziona kwa ukaribu utaelewa kwamba si kila kitu kina fanana na kionekanavyo.  Ila mpaka kuamua kukusanya na mabegi na kuondoka kwenye ‘jumba kali’? Majubu yake yalikua ya moja kwa moja tu na nafsi yake ilikua tayari kuhamia nyumba nyengine mwenzangu. Natumai kwa kiasi flani utasoma jambo, ingawa kwangu mimi natamani ningepata zaidi na zaidi ila inaonekana bado hakua tayari kutufungukia mazima. Binafsi namshkuru kwa kuja mezani kwetu na pengine tutaweza kukutana tena mbeleni In Shaa Allah. Yangu matumaini bado utaokota mawili matatu. Love, Salama. --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support
 • Salama Na podcast

  Ep. 48 - Salama Na JK | MSOGA UNO

  1:01:47

  Muda si mrefu iliopita nilirudi nyuma kidogo kwenye kumbukumbu ya mawasiliano ya kwanza kabisa kati yangu na moja wa wasaidizi wake Mheshimiwa Jakaya Mrisho wa Kikwete na hiyo ilinirudisha nyuma mpaka mwezi wa tatu mwaka 2020. Kama mtu mwengine yoyote hii ilikua ndoto tu ambayo kwa Rehema na Baraka za Allah ilibidi itimie. Kwa Baraka zake hizo mimi na wenzangu tunashkuru sana sana kwa kuweza kulikamilisha hili. Shukran za dhati ziende kwa Doris Mollel ambaye kwa msaada wa Sadam ‘Almando’ Sanare alinimbia Doris anaweza akatu unganisha na mmoja wa wasaidizi wake ili tuweze kuona kama tunaweza pata hii nafasi, na kama ujuavyo, mengine yote yamebaki kuwa historia tu tena, maana yametimia. Mimi kama wewe tu, shabiki nambari moja wa Jakaya Mrisho Kikwete na kukutana naye, kukaa naye chini na kuweza kumuuliza maswali tuliyokua tumeyaandaa (kwa muongozo wao) ilikua raha isiyoelezeka. Mzee charming, mwenye roho nzuri na muelewa kabisa. Mengine yalofuata baada ya hapo ndo ambayo utayaona au kuyaskiliza katika maongezi yetu haya. Mengi yalikua ni juu ya yeye alivyokua na uelewa wake kwenye mambo mengi. I wish tungeweza kuongea nae kuhusu masuala meeengi zaidi kuhusu kiila kitu ila ki ukweli hii inatosha kwa sasa na Mungu atajaalia tutakutana naye tena siku nyengine In Shaa Allah. Mheshimiwa JK aliongea nasi kuhusu Wazazi wake, elimu, uelewa wake wa mambo, yeye kuwa mwanajeshi. Jinsi alivyokutana na Mama Salma. Historia ya nyuma kidogo kuhusu mapenzi na jinsi Marehemu Mzee wake alivyomtaftia mke na kuzaliwa kwa mtoto wake wa kwanza ambaye ni Ridhwan. Kuhusu kitabu chake, mapenzi yake na basketball na muziki. Pia Kobe Bryant na mapenzi kwa wajukuu zake. Kama ilivyo kawaida yetu, yangu matumaini utapata kadhaa humu ya kukufunza jambo. Na napenda kuchukua nafasi hii kumshkuru kila mtu ambaye alisaidia hilo kutimia na zaidi team yangu yote ya ‘YahStoneTown’ ambayo ilifanya kazi iliyotukuka kukamilisha hili. Nikutakie Kheri ya mwaka mpya na kila lenye Kheri nawe. Enjoy. Love, Salama. --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support
 • Salama Na podcast

  Ep. 47 - Salama Na JOTI | SIMPLY SPECIAL

  1:19:35

  Lucas Mhaville ni maalum sana, kwa ki vyovyote vile utakakavyotaka wewe, ki maisha, ki muonekano, ki uelewa na jinsi anavyokua mpya kila siku kwenye ulimwengu wake, jinsi anavyo jipa matawi na kujigawa kisanaa. Jinsi anavyotoa character wapya kila mara kwaajili tu ya kuleta ladha mpya kwenye sanaa yake, hili linamfanya aendelee kuwa mchekeshaji pekee kwenye kizazi chetu ambaye huwezi kuona amechuja au hana jipya kwenye kukufurahisha wewe. Kabla sijaiandika hii, kipande kidogo cha video kilienda kwenye ukurasa wangu wa Instagram (@ecejay) kwaajili ya kuwafahamisha watu kwamba JOTI atakua ndo mgeni wetu wa usiku wa leo, na kwenye hiyo video nilimuuliza kuhusu kabila lake ambalo kwa mujibu wake ni kabila dogo tu kutoka huko Morogoro na yeye na Baba yake mdogo ambaye ni Polisi ndo watu waarufu zaidi, ila kwa wingi wa replies kutoka kwa watu wengi wa kabila hilo inaonyesha si kabila dogo kama yeye alivyodhani, ila hiyo ni tisa, kumi ni jinsi ambayo watu WANAMPENDA na kusikiliza KILA ANACHOSEMA, hiko ni kipawa tofauti kabisa, sio kila mtu anaweza kuwa na uwezo huo. Yeye ni mzaliwa wa Morogoro na alikuja Dar es Salaam baada ya mzazi wake mmoja kufariki, alichukuliwa na ndugu yake na kuja kulelewa hapa, amesoma hapa na sanaa yake pia ilianzia hapa alipokua shuleni. Nani alimsukuma? Na je alisoma mpaka daraja lipi? Mimi na yeye pia tunazungumzia umuhimu wa elimu na malezi bora. Maisha yake alipokua mdogo na mafunzo aliyoyapata growing up. Joti si wa leo, akiwa na miaka yake 38 anajielewa vizuri sana tu. Maongezi yetu pia yalitupeleka kwa uanzishwaji wa kundi la Original Comedy ambalo lilitufanya sote tuwapende sana na enzi hizo za EATV wao wanapokua hewani basi nchi nzima ilikua inasimama kwaajili ya kuangalia walichotuandalia. Yalikua mafanikio haswa! So nini kilitokea mpaka wakaomdoka EATV? Na wao kama kundi kuna lolote kwa sasa? Au kila mtu ndo solo? Na vipi kuhusu Vengu? Yule mwenzao (mwenzetu) ambaye alipata matatizo makubwa ya ki afya na mpaka naandika hii bado yuko kitandani? Shida yake hasa ni nini? Haina tiba? Humu pia tumeongelea mahusiano yake na Seki, ambaye alikua naye toka enzi za OC akiwa kama kiongozi na mtayarishaji. Mahusiano yake na Mpoki, Masanja ambaye sasa amejikita kwenye masuala ya ki kanisa, Wa Kuvanga na McRegan? Wako wapi? Kama kuna comeback ya kundi? Lini? Wakati nafanya hii pia nilitiwa elimu na Director wangu wa siku hiyo (Ms Lydia Igarabuza) kwamba, ukitaka kuongea na mchekeshaji, ili upate utakacho, basi usimpe nafasi ya yeye kukuchekesha mpaka ukasahau kilichomleta pale, namshkuru sana kwa hilo maana nadhani ki kawaida kama wana tungecheka zaidi kabla ya kuyasikia yote ambayo tumeongea humu. Respect nyingi ziende kwa Joti ambaye ameweza ku maintain status yake ya heshima ya juu kwenye kazi yake, na kama binadamu. Yangu matumaini utaokota mawili matatu hapa ambayo yatazidi kukutia mafuta ya kukufanya utake maendeleo zaidi na heshima kwenye jina lako na maisha yako. Tafadhali enjoy. Love, Salama --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support
 • Salama Na podcast

  Ep. 46 - Salama Na HK | NJE YA BOX KIDDOGO

  1:34:38

  Sikuwahi kuujua ufahamu wa Dr Hamisi Kingwangala kwenye suala la dini kwa kiasi ambacho ameniambia wakati tunaongea kwenye kikao chetu hiki, na alinilelezea kwa majina yake ya kizuoni huku akiniambia nini kwa binafsi yake anaweza kukifanya kwa kituo pale anapotaka, lakini pia aliniambia juu ya suala la yeye kutokua anaswali sala tano kama ilivyokua zamani na kwamba si jambo analojivunia asilan! Hii ilikua mara yangu ya pili kukutana na kuongea nae kwa kituo, kama ilivyokua kwa Taji nae pia niliongea naye miaka ya nyuma wakati nafanya Mkasi, na kwa kuongea naye round hii nimejifunza kwamba hawa ni kama watu wawili tofauti kabisa na si kwa ubaya, yule wa kwanza alikua si muongeaji kama huyo wa sasa  kwasababu amekua kwa kiasi flani na kukua ni jambo ambalo sisi wenyewe na wazazi wetu huangalia kwa makini kuanzia pale ulipokua tuseme miaka mitano iliyopita na sasa na mipango na maratajio yako. Kwa hili Sheikh HK kaserebuka nalo vizuri tu. Hakuna mtu asiyemfahamu Hamis Kingwangala ndani ya nchi hii na nje, jinsi ambavyo alifanya kazi nzuri ya kampeni ya kuitangaza Tanzania duniani kwa umaarufu wa vivutio vya utalii wetu na utajiri wa nchi yetu pendwa. Alichukua muda huo pia kutembelea karibu mbuga zote na nchi hii na wakati huo huo kupambana na majangili na waharibifu wa wanyama pori, vita ambayo ilikua ndo stori ya kipindi flani hapo nyuma. Yeye HK alikua anamalizana na maneno ya walimwengu ambao walikua wanaongea mengi kwenye mitandano ni kwa  yeye. kuendelea kupiga  kazi yake vizuri tu mpaka akamaliza miaka mitano ya kwanza ya Rais aliyempa cheo hicho kwa usalama tu, nasema hivyo kwasababu kuna wengi ambao walikua wanateuliwa lakini siku zao za kukaa ofisini hazikua nyingi sana ila HK aliweza kuendana vizuri na mawimbi kwenye bahari ya uongozi ambayo bila ya shaka ilikua na mitihani yake. Pia umaarufu wake mwengine Bwana HK ulikuja baada ya kuwa ntumiaji mzuri sana wa Twitter, sehemu ambayo huitumia kwa kufanyia kazi yake ya kuitangaza nchi na pia kumalizana na ‘wabaya’ wake wote ambao wamekua wakila nae sahani moja kila mara panapokua na jambo ambalo yeye amesema au kuwakilisha mooni yake juu ya suala flani. HK hana tabia ya kuona haya kumjibu mtu ambaye kwa namna moja ama nyengine anakua kamgusa pale alipokua hapataki yeye au pengine tofauti tu ya mawazo, muda mwengine utakuta watu wamefika huko. Kubwa kuliko ilikua hii ya mwaka huu ambayo alihoji juu ya uteuzi wa CEO mpya wa klabu yake pendwa ya Simba na pia suala la mwekezaji kutimiza ahadi yake ya kuipa Simba shilingi bilioni 20 za kuendeleza klabu. Hili suala liliamsha zogo kubwa kati ya HK, muekezaji wa klabu pamoja na mashabiki wa Simba, lilifanya pia tujue siri za ndani za kibiashara kati ya wawili hawa na jinsi ambayo wote wawili walivyokua wanajibizana mitandano ilifanya watu wengi wanyanyue nyusi kwa mshangao na kujuzwa mambo ambayo pengine yalikua hayana faida kwa watu wengine kujua. Hivi karibuni wawili hawa walimaliza tofauti zao huko huko kwenye mitandao hiyo hiyo ya kijamii kama walivyofanya awali. Niloitaka kujua kama kuna muendelezo wa hayo maongezi yao, kama walishakutana toka majibizano yale yatokee, pia tuliongelea ajali ambayo aliipata akiwa kazini na ambayo pia ilizungumziwa na watu wengi. Pia niliongea nae kuhusu Rais Magufuli, uchaguzi wa mwaka huu ambao chama chake kimeshinda  kwa ushindi mnono na jinsi ambavyo hakupata nafasi kwenye baraza la mawaziri na manaibu wake ambalo limeundwa hivi karibuni na ambavyo aliipokea taarifa hiyo. HK ni mtu poa sana, kijana ambaye ni Kiongozi, Baba, Kaka na mfanyabiasha mzuri tu ndo darasa letu la wiki hii na yangu matumaini kana kawaida atakua na jambo la kukufunza kwahiyo tafadhali enjoy. Love, Salama. --- Support this podcast: https://anchor.fm/yahstonetown/support

Get the whole world of podcasts with the free GetPodcast app.

Subscribe to your favorite podcasts, listen to episodes offline and get thrilling recommendations.

iOS buttonAndroid button
© radio.de GmbH 2022radio.net logo