Salama Na podcast

Ep. 49 - Salama Na MAVOKO | WINGMAN

1/14/2021
0:00
1:05:30
Rewind 15 seconds
Fast Forward 15 seconds

Kwa muda mrefu nimekua nikitaka kuongea na Mavoko ila ratiba zetu zilikua hazijawahi kuwa sawa na hivyo tukawa tunapishana tu. Kama mimi sina program naye basi yeye atakua free, na mimi nikiwa free basi yeye atakua na mipango ya kutoa kazi mpya ambayo itanifanya ningoje ili viende pamoja, au atakua kasafiri, au mimi nitakua nishaset watu wengine, ilikua kama tunacheza kidali po ila katikati ya mwezi wa kumi na mbili hatimaye yakatimia.

Hakuna doubt juu ya uwezo wake popote pale utakapoenda ingawa baada ya yeye kuamua kuondoka kwenye label ya WCB kulikua na mengi yalosemwa na kutendwa na baadhi ya mashabiki yalikua yanaweza kukuaminisha jambo na mpaka kufikia pengine ku doubt huo uwezo wake. Mambo mengi yalisemwa, ya kusikitisha, ndoa haikuvunjika vizuri ila ambacho nilikiona kwake ni ustaarabu wa hali ya juu, wa kuwaacha walimwengu waseme na kufanya watakayo huku yeye akiwa ame focus kwenye kipaji chake na kujipanga upya.

Moto wa Mama Richard anaujua mziki mwingi, ana uwezo mkubwa wa kuimba na kuandika na kucheza pia, ila kabla hajaingia kwenye label alikua anajulikana tu, ila kumfahamu vizuri na kuthamini kipaji chake kulikuja baada ya yeye kushirikiana na mmoja kama si msanii bora zaidi kuwahi kutokea na kuipeperusha zaidi bendera ya Tanzania ndani ya Diamond Platnumz. Ushirikiano wao ulitupa ‘anthem’ kadhaa ambazo mpaka leo ukiziskiliza hazichuji. Ilikua kama team ya wenye vipaji pekee, kama ni mfuatiliaji wa mpira wa kikapu hii tunaweza kuifananisha na ile zile team mbili za Mashariki na Magharibi ambazo zinakusanya wachezaji wenye uwezo wahali ya juu.

Saasa, ikawaje hasa mpaka akaona aachane na all star hiyo na kupeleka team yake uwanjani akiwa solo? Nini hasa kilifanya mpaka afikie maamuzi hayo? Kuna mtu au kitu kilimshinikiza? Je yalikua maamuzi sahihi? Pia kuna masuala binafsi ya kifamilia na suala la yeye kutomfahamu Baba yake takati anakua, elimu yeke, ndugu zake, Mama yake na muziki ulichomfanyia katika maisha yake.

Mavoko huyu ambaye mimi namfahamu nilikutana naye Kampala, Uganda kama maka saba iliyopita na mazungumzo yetu yalikua yanahusu kipaji chake na jinsi ambavyo nilikua naona ‘hapewi’ nafasi maana kama ngoma zake zilikua nzuri tu, video ndo usiseme ila hakuna na spotlight aliyokua anastahili, peleka mbele miaka mpaka 2021 ambapo alipata nafasi kwa miaka takriban miwili na nusu kufanya kazi na lebo bora zaidi ila baada ya muda akaamua kubwaga? Kwanini hasa? Sote tunajua kama nyasi za jirani huonekana zimestawi kweli kweli ila ukifika na kuziona kwa ukaribu utaelewa kwamba si kila kitu kina fanana na kionekanavyo. Ila mpaka kuamua kukusanya na mabegi na kuondoka kwenye ‘jumba kali’?

Majubu yake yalikua ya moja kwa moja tu na nafsi yake ilikua tayari kuhamia nyumba nyengine mwenzangu. Natumai kwa kiasi flani utasoma jambo, ingawa kwangu mimi natamani ningepata zaidi na zaidi ila inaonekana bado hakua tayari kutufungukia mazima. Binafsi namshkuru kwa kuja mezani kwetu na pengine tutaweza kukutana tena mbeleni In Shaa Allah. Yangu matumaini bado utaokota mawili matatu.

Love,

Salama.

--- Support this podcast: https://podcasters.spotify.com/pod/show/yahstonetown/support

More episodes from "Salama Na"