Salama Na podcast

Ep. 48 - Salama Na JK | MSOGA UNO

1/7/2021
0:00
1:01:47
Rewind 15 seconds
Fast Forward 15 seconds

Muda si mrefu iliopita nilirudi nyuma kidogo kwenye kumbukumbu ya mawasiliano ya kwanza kabisa kati yangu na moja wa wasaidizi wake Mheshimiwa Jakaya Mrisho wa Kikwete na hiyo ilinirudisha nyuma mpaka mwezi wa tatu mwaka 2020. Kama mtu mwengine yoyote hii ilikua ndoto tu ambayo kwa Rehema na Baraka za Allah ilibidi itimie. Kwa Baraka zake hizo mimi na wenzangu tunashkuru sana sana kwa kuweza kulikamilisha hili.

Shukran za dhati ziende kwa Doris Mollel ambaye kwa msaada wa Sadam ‘Almando’ Sanare alinimbia Doris anaweza akatu unganisha na mmoja wa wasaidizi wake ili tuweze kuona kama tunaweza pata hii nafasi, na kama ujuavyo, mengine yote yamebaki kuwa historia tu tena, maana yametimia.

Mimi kama wewe tu, shabiki nambari moja wa Jakaya Mrisho Kikwete na kukutana naye, kukaa naye chini na kuweza kumuuliza maswali tuliyokua tumeyaandaa (kwa muongozo wao) ilikua raha isiyoelezeka. Mzee charming, mwenye roho nzuri na muelewa kabisa. Mengine yalofuata baada ya hapo ndo ambayo utayaona au kuyaskiliza katika maongezi yetu haya. Mengi yalikua ni juu ya yeye alivyokua na uelewa wake kwenye mambo mengi. I wish tungeweza kuongea nae kuhusu masuala meeengi zaidi kuhusu kiila kitu ila ki ukweli hii inatosha kwa sasa na Mungu atajaalia tutakutana naye tena siku nyengine In Shaa Allah.

Mheshimiwa JK aliongea nasi kuhusu Wazazi wake, elimu, uelewa wake wa mambo, yeye kuwa mwanajeshi. Jinsi alivyokutana na Mama Salma. Historia ya nyuma kidogo kuhusu mapenzi na jinsi Marehemu Mzee wake alivyomtaftia mke na kuzaliwa kwa mtoto wake wa kwanza ambaye ni Ridhwan. Kuhusu kitabu chake, mapenzi yake na basketball na muziki. Pia Kobe Bryant na mapenzi kwa wajukuu zake.

Kama ilivyo kawaida yetu, yangu matumaini utapata kadhaa humu ya kukufunza jambo. Na napenda kuchukua nafasi hii kumshkuru kila mtu ambaye alisaidia hilo kutimia na zaidi team yangu yote ya ‘YahStoneTown’ ambayo ilifanya kazi iliyotukuka kukamilisha hili.

Nikutakie Kheri ya mwaka mpya na kila lenye Kheri nawe.
Enjoy.

Love,
Salama.

--- Support this podcast: https://podcasters.spotify.com/pod/show/yahstonetown/support

More episodes from "Salama Na"