Salama Na podcast

SE7EP34 - SALAMA NA FETTY DENSA | KUTOKA UBAVUNI...

2023-02-02
0:00
1:12:18
Spola tillbaka 15 sekunder
Spola framåt 15 sekunder

Kwa ambao wanafuatilia mpira hapa nyumbani wanamjua mchezaji huyu mahiri wa Simba Queens lakini ambao wanafuatilla soka la wanawake hawa watakua wanaelewa uwezo binafsi na uhodari wake wa kucheza namba tofauti tofauti uwanjani ila ukimkuta kaikamata mbavu ya kulia aidha kwa Simba au timu ya Taifa ya Tanzania. Fatuma Issa ni mtu na nusu, hakuna mpenzi wa mpira au kocha yoyote wa mpira anaweza akamuacha kwenye benchi wakati team inatafuta matokeo au inataka kuwaonyesha walofika kuwaangalia vipaji ambavyo wanavyo kwenye kikosi chao. Kwa yoyote yule na kwa vyovyote vile, Fetty Densa, ni lazima AANZE.

Ananikumbusha sana mimi na rafiki zangu wakati tunakua, tulikua chizi michezo hasa baada ya kufika shule ya Sekondari, ilikua kama lazima kila mmoja kuwa na uwezo wa kucheza zaidi ya mchezo mmoja ili tuwe na vikosi imara inapotokea kwenda kufanya uwakilishi wa shule, mkoa au nchi. Binafsi nilikua na uwezo wa kucheza Basketball na table tennis tu ila nina marafikia kama kina Kalova na Mboni Mntambo ambao wao walikua wanacheza Basketball, Netball, Volleyball na chochote kitakajokuja mbele ambacho kinatumia mpira kucheza lol, na tena VIZURI, sio kujazia namba tu uwanjani. Naye Fetty ni kama wanangu hao kutokana na maongezi yetu. Ananiambia hata shuleni mwalimu na wanafunzi wote katika shule yao walikua wakifahamu na kujivunia yeye sana.

Akiwa anakua huko Morogoro Fetty ni ‘mtoto wa Bibi’ zaidi, yeye ndo alomlea na kumtunzia siri zake zote, na ndo alomfundisha kupika na kumkumbusha kwamba yeye ni mtoto wa kike kwahiyo alihakikisha pia mjukuu wake kwenye masuala ya kupika na usafi wake na wa nyumba pia haachi kujifunza. Bibi pia ndo alipewa ahadi ya kwamba kuna siku mjukuu atakuja kuwa mchezaji hodari kuwahi kutokea hapa nyumbani na so far, so good. Babu yake nae hakua nyuma kwenye kumsifia mjukuu wake pale anapofanya vizuri jikoni kwasababu pengine kuna umuhimu wa kufanya hivyo ili ampe moyo mjukuu wake.

Fatuma anatuambia humu kwenye maongezi yetu jinsi ambavyo alihangaika mkoani Morogoro kupata team ya kucheza na jinsi ambavyo alijutuma toka siku ya kwanza kuhakikisha ndoto zake zinatimia. Ukimsikiliza kwa makini utagundua kama ni mtu mwenye mawazo ya mbele kuliko hata umri wake, hiyo inamsaidia pia inapofika wakati wa kufanya maamuzi anapokua ndani na nje ya uwanja. Unaweza ukajiuliza kwa kipaji chake na ujuzi wake kwanini hachezi nje ya nchi? Kwanini amekua Simba huu msimu wake wa nne na amekua akicheza kwa kiwango cha juu sana? Densa anatupa majibu ya swali hilo ambalo nina uhakika wengi wao wamekua wakijiuliza.

Mahusioano yake na Mama yake ambaye alikua mmoja kati ya wanenguaji wazuri miaka iliyopita na ndo alimfanya pia mwanae naye atake kuwa Densa (ndo jina la Fetty Densa lilikotokea). Wana mahusiono ya aina gani? Mama alilichukuliaje suala la Binti yake kuchagua soka? Na Mzee wake nae yuko wapi? Nafasi yake kwenye team yake? Team ya Taifa je? Experience ambayo waliipata Morocco wakati Simba ilipoenda kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa barani Africa? Vipi kuhusu mpira wa miguu wa wanawake hapa nyumbani? Pesa ipo? Muelekeo je?

Haya maongezi ni moja ya maongezi bora ambayo nimeshawahi kufanya na natumai yatafungua milango kwa watoto wa kike na wazazi wao wengi kuelewa na kuipambania fursa hii ambayo Dunia nzima imeanza kuielewa.

Tafadhali enjoy.

Love,

Salama.

--- Support this podcast: https://podcasters.spotify.com/pod/show/yahstonetown/support

Fler avsnitt från "Salama Na"