Ulikua muda mwingi hasa umepita toka mara ya mwisho nilionana na Evans wa Bukuku na kukaa naye chini kisha tukaongea. Na ki ukweli hajawahi kuwa rafiki yangu wa karibu ila ni mtu ambaye tunafahamina na kuheshimiana. Hustle zake nazifahamu kwa ukaribu maana industry ambayo tunafanya kazi ndo hiyo hiyo kwahiyo nikama chakula, tusipokutana jikoni basi tutakutana kwenye sahani. Kama ilivyo kwa watu wengi nimekua nikimsikia kwenye radio mbali mbali katika safari yake kama mtangazaji wa vipindi mbalimbali lakini pia nimekua nikimuona kwenye majukwaa mbalimbali akifanya shughuli zake za ku host sherehe au matamasha kadhaa.
Kwenye kitabu changu yeye ni mmoja wa hustlers timamu kabisa ambao Tanzania yetu inayo na mazungumzo yetu haya pia kwa kiasi kikubwa yamenipa picha nyengine ya aina ya mtu ambaye yeye ni, kwanza alikuja kwenye set na binti yake (ambaye tayari kashanizidi urefu) na inavyoonekana ni rafiki yake mkubwa maana huwa yuko naye benet mara nyingi, nadhani kwa experience yake ya kukutana na watu wengi kutoka sehemu tofauti kumemfanya naye pia ajifunze mambo flani kutoka kwao na hili ni jibu kati ya majibu ambayo niliyapata kutoka kwenye maongezi yetu. Watu wengi ambao amekua akikutana nao wanamfundisha mambo mengi na ukiachana pia kwamba na yeye amekua kwenye maisha ya ‘ki familia’ zaidi maana yeye na wazazi wake na Dada pamoja na Marehemu Kaka yake wako karibu sana.
Moja ya mambo aliniambia ni jinsi ambavyo anaangalia anachokula na kujitunza yeye na mwili wake, anahakikisha anapata muda mzuri wa kupumzika na vilevile kufanya mazoezi. Anajua umuhimu wa haya yote na anayafanyia kazi. Binafsi kwanza nilitaka kujua kwanini amekua akimua kufanya vipindi vya radio vya asubuhi tu na sio wakati mwengine? Nini hasa maana ya hiyo? Majibu yake yatakufurahisha kama nawe utakua mtu wa kujifunza.
Hatukuweza kuacha kumuongelea Marehemu Roy ambaye alikua ni Kaka yake, nami nilijua hiyo siku, muda wote nilikua nikidhania yeye ndo mkubwa. Roy ni mmoja wa wapishi wazuri wa Bongo Flava tamu ambayo tulianza kuipenda kwenye miaka ya mwanzo ya 2000, Roy ndo mpishi wa Mr Blue, kina Ally Kiba, kina ParkLane na wengine tele, heshima yake ni kubwa na binafsi nilitaka aliskie hilo kutoka kwangu. Na nilitaka kujua kitu ambacho kilisababisha kifo chake pia, haikua rahisi kuuliza maswali kama haya lakini pia hakukua na budi maana maua ya Kaka yake ilikua ni wajibu wake kuyapokea.
Pia tulimuongelea Enika ambaye ni Dada yake pia, nilitaka kujua nini ambacho kimemfanya asifanye tena Bongo Flava, na nini ambacho anafanya sasa, na je ana furaha? Tuliongelea pia hustle yake nyengine ya comedy ambayo nayo amekua akiizingatia na kuisimamia kwa miaka sasa, hakuna comedian yoyote kwenye nchi hii ambaye kwa kiasi chochote kile hana mchango wake ndani yake, na si lazima awe amepita mikononi mwake, bali hata njia (nyingi) ambazo amewahi kuzitengeneza na ambazo anaendelea kuzisimamia.
Evans mtu, tena wa watu na yangu matumaini utakubaliana nasi mara tu baada ya kuangalia au kuskiliza maongezi yetu haya.
Tafadhali enjoy.
Love,
Salama.
--- Support this podcast: https://podcasters.spotify.com/pod/show/yahstonetown/supportOtros episodios de "Salama Na"
No te pierdas ningún episodio de “Salama Na”. Síguelo en la aplicación gratuita de GetPodcast.