Salama Na podcast

Ep. 51 - Salama Na Babu Tale | JUGGLER

1/30/2021
0:00
1:16:40
Rewind 15 seconds
Fast Forward 15 seconds

Hamis Tale Tale ni MWAMBA wa maisha yake na ya wale walomzunguka kwa miaka nenda miaka rudi na kutoka upande huu wa muandishi na mtangazaji ni heshima tu kwenda mbele. Kuna msemo mmoja wa Kiswahili kuhusu nyani ambaye unamkuta mjini. Ya kwamba anakua kashakwepa MISHALE ya kutosha kwahiyo unapomkuta town inabidi umpe heshima zake za kutosha.

Kwa waasisi wa Bongo Flava jina lake kuwa juu pale na haiwezi kuwa kosa hata kidogo na kuna wasanii kibao ambao wana mshutumu kwa mambo mengi lakini kuna wale ambao hawawezi kumsahau maishani mwao kwa sababu ya mchango mkubwa ambao amewapa. Na vile vile ukimtaka mtu wa kukuelezea tabia na uzuri wa watu wa iaina zote katika industry hii basi Babu Tale ndo ambaye atakuelezea hilo kwa kinaga ubaga maana akiachana na ucheshi wake, Tale pia ni msimuliaji habari mzuri tu.

So kuanzia kwa Marehemu Kaka yake Abdu Bonge mpaka kwa huyu anayevaa kaunda suti zilizonyooka ndo sisi tulipopataka, ametoka umbali gani? Haya yote aliyonayo ilikua ndo mipango yake? Ki ukweli mmoja kama anaamini ya kuwa kuna yatu wanakua wamekaa tu wanaangalia progress zeta kwa mbali na kuona haswa umbali gani watu wametembea mpaka kufika kwa mfano ambapo Tale amefika basi bila ya shaka atakua ametia nne yake huku akiwa kapendeza sana na kumpigia makofi tu kwa yale aliyoweza kuyafikia mpaka sasa. Ukichukulia huyu ni Kijana ambaye kuna wakati flani katika maisha yake ilikua inabidi asubiriane na mmoja ya ndugu zake ili waweze kubadilishana aidha viatu au uniform ili na yeye aweze kwenda shule!

Nimekutana na watu wengi katika maisha yangu na Tale yeye yake tabia ni kutokua na breki pale anapokua na lake, yale mambo ya sijui kulainisha maneno ili pengine asikuumize hisia zako yeye hana, kinda like me, la kusemwa lisemwe kisha maisha yaendelee, na hiyo ni kwa kumtakia mtu mema tu, pia anachekesha na anapenda kucheka pia, also… Mkali, sio wa ‘kulealea’, sio babysitter hata kidogo na hiyo yote ni kwa kutaka JEMA kwa mtu ambaye anamsimamia. Najua kama binadamu atakua na mapungufu yake na hayo ndo yako pia kwenye maneno ya baadhi ya wasanii ambao ameshawahi kufanya nao kazi.

Tale ana khadithi ya kila mmoja wetu kwenye kiwanda hiki cha muziki na burudani na nna uhakika miaka kadhaa ya mbele atakua na khadithi za wanasiasa wenzake na viongozi ambao kuanzika mwaka huu anaanza kuwa nao kwa muda mrefu kwenye maisha yake.

Mwaka jana Babu Tale alimpoteza mke wake kipenzi ambaye alitangulia mbele ya haki na kumuachia watoto ambao sasa yeye ndo anaye waangalia kwa msaada pia wa baadhi ya ndugu zake. Hii ilikua habari nzito kwa kila mtu, mke wake amble wengi tulikua tunamfahamu zaidi kupitia mitandano ya kijamii, mimi nishawahi kukutana naye mara kadhaa, alikua Mrembo sana wa sura na roho, Mwenyezi Mungu Amrehemu. Mengi sana yalisemwa na kwa ufahamu wangu nikaona basi hakuna wa kutuambia ambayo tunadhani tuna haki ya kuyajua zaidi yake YEYE. Nini haswa kilitokea?

Natumai maongezi yetu haya yatakupa somo flani kwa mambo kadhaa ambayo tunakutana nayo maishani mwetu, Tale amanitajia watu ambao kwa kiasi kikubwa wanamsaidia kumpa faraja baada ya mkewe kutangulia mbele ya haki, na watu hao hata sio NDUGU ZAKE, ingawa najua nao kwa kiasi chao wanamsaidia ki vyao. Hili kwangu liliingia haswa.

Humu kuna mengi tuliyagusia na hakua na hiyana kutuambia mawazo yake na kwa hilo napenda kumshukuru. Tafadhali enjoy session hii ambayo kama kawaida natumai itakufunza mambo mawili matatu, iwe kuhusu mapenzi, maisha, kazi, watoto, muziki, marafiki na hata siasa, Na pengene hata jinsi ya kukimbiza naoto zako!

Love,
Salama

--- Support this podcast: https://podcasters.spotify.com/pod/show/yahstonetown/support

More episodes from "Salama Na"